Mwandishi:
Dkt. Benjamin M, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
22 Machi 2020, 12:37:22
Matibabu ya nyumbani ya Bruizi| ULY CLINIC
Bruizi ni neno la tiba linalotumika na ULY CLINIC, neo hili lilitokana na neno la kitiba "bruise" ambalo lilitoholewa kutoka kwenye neno la kifaransa "bruiser" linalomaanisha "kupasuka"
Katika tiba neno “bruise” linatumika kumaanisha kupasuka kwa mishipa midogo ya damu maeneo chini kidogo ya ngozi na kusababisha damu kuvilia na kuonyesha rangi nyeusi, zambarau au ya bluu chini ya ngozi ambayo hubadilika jinsi siku zinavyoenda.
Matibabu ya kuvia damu
Matibabu ya nyumbani ya kuvia kwa damu chini ya ngozi(bruizi) yanayoshauriwa na ULYCLINIC ni ;
Pumzisha eneo lenye bruizi kwa muda kiasi.
Tumia barafu kukanda eneo lililovia damu, weka barafu katika taulo, acha kwenye eneo lililovia kwa dakika 10 hadi 20. Rudia kufanya hivi mara kadhaa kadiri unavyoweza angalau mara tatu kwa siku, kwa muda wa siku nne toka umevilia damu
Gandamiza eneo lililovimba kwa kutumia bandeji ya mpira, usikaze sana kuzuia kuziba mishipa ya damu ya chini zaidi.
Weka eneo lililo na shida juu kidogo ya usawa wa moyo, unaweza kutumia mto au kitu kingine ambacho kinaweza kukusaidia kunyanyua sehemu iliyovilia damu
Kama kuna mpasuko kwenye ngozi, hauhitaji kuuziba kwa bandeji, Tumia dawa za kupunguza maumivu kutoka kwenye maduka ya dawa baridi kama ni lazima
Wakati gani wa kuwasiiliana na daktari?
Endapo una bruizi pamoja na dalili au mambo yafuatayo ni vema ukamwona daktari wako kwa uchunguzi zaidi;
Kuna maumivu makali kwenye eneo lenye bruizi
Bado unapata maumivu makali siku tatu baada ya kupata jeraha dogo
Bruzi imetokea bila sababu ya msingi
Una bruizi kubwa, au zinazotokea mara kwa mara, zilizo usoni au mgongoni
Unapata bruizi kirahisi au una historia ya kutokwa na damu kirahisi mfano kama
Umekwanguliwa kidogo, damu zinatoka muda mrefu kuliko mtu mwingine akiwa na jeraha kama lako.
Una historia ya kutokwa na damu kwenye fizi kirahisi unapopiga mswaki au puani bila sababu.
Una matatizo ya kutokwa na damu/magonjwa
Kuwa na historia kwenye familia ya kutokwa na damu kirahisi.
Kumbuka.
Mambo haya yaliyoorodheshwa hapa yanaweza kumaanisha una maatizo katika damu na hivyo ni vema kuwasiliana na daktari wako mapema
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasilianane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga namba za simu au kubonyeza sehemu imeandikwa "Pata tiba" chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
21 Julai 2023, 16:20:09
Rejea za mada hii;
1. Muscle contusion (bruise). American Academy of Orthopaedic Surgeons.
http://orthoinfo.aaos.org/topic.cfm? topic=A00341. Imechukuliwa 10.03.2020.
2. Approach to sports injuries. Merck Manual Professional Version.
http://www.merckmanuals.com/professional/injuries-poisoning/sports-injury/approach-to-sports-
injuries. Imechukuliwa 10.03.2020.
3. Buttaravoli P, et al. Contusion (bruise). In: Minor Emergencies. 3rd ed. Philadelphia, Pa.: Mosby
Elsevier; 2012. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.03.2020.
4. Kraut EH. Easy bruising. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 10.03.2020.
5. Majibu kutoka kwa wataalamu wa ULY CLINIC